Habari Za Un

Asante IFAD kwa kutuwezesha watu wenye ulemavu Liberia

Informações:

Sinopsis

Nchini Liberia, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD umejengea uwezo watu wenye ulemavu wa kuona na kuwawezesha kuongeza vipato na vile vile uhakika wa kupata chakula. Simulizi ya Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM mkoani Mwanza nchini Tanzania, inaelezea zaidi.Tuko kaunti ya Lofa, kaskazini kabisa mwa Liberia, magharibi mwa Afrika, tunakutana na Hawa Kamara, yeye ni mlemavu wa kutoona. Yeye pamoja na wenzake wa chama cha watu wenye ulemavu wa kutoona hapa Lofa, wanathibitisha kuwa unapoamua kufanya kitu, hakuna kinachokuzuia.Kupitia mradi wa Mabadiliko ya kilimo kwa wakulima wadogo na uchechemuzi wa kilimo biashara au STAR-P, mavuno ya mpunga kwenye shamba la kikundi hicho, yameongezeka kwa asilimia 300.Hawa anasema, “Mwanzoni hatukuwa na kitu kabisa. Tulihangaika sana kulima mpunga. Lakini baada ya IFAD kutufikia katika maisha yetu na kutusaidia, mambo yalianza kubadilika. Walitupatia pembejeo na mbegu za ubora wa juu kuanzisha mashamba. Tulitumia mbegu hizo ku