Jua Haki Zako

Wazee na Wasiojiweza wafaidika na Mpango wa Makazi Bora Nchini Kenya

Informações:

Sinopsis

Maelfu ya wazee, walemavu, na wajane nchini Kenya wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa za makazi duni, hasa katika maeneo kame. Hali hii imewalazimu wengi kuishi katika mazingira yasiyofaa, huku baadhi yao wakikosa makazi kabisa. Hata hivyo, mpango wa kuwajengea makazi bora umeanzishwa katika kaunti mbalimbali, ukiwapa matumaini wapate hifadhi salama na yenye hadhi. Katika kijiji cha Naibor, Kaunti ya Laikipia, baadhi ya wazee tayari wameanza kunufaika na mpango huu.