Habari Za Un
Mafanikio ya Mradi wa ACP MEAs 3 Rwanda katika kuboresha kilimo endelevu
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:03:40
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika kilimo pamoja na usimamizi salama wa viuatilifu. Hili linafanyika kupitia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ACP MEAs 3 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU. Mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kuhamia kwenye mifumo ya kilimo endelevu kimazingira na kuwajengea uwezo wa utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira. Sharon Jebichii anatupeleka nchini humo kumulika mradi huo..