Habari Za Un

Akili mnemba na watu wenye ulemavu ni moja ya ajenda za COSP18 tutakazozingatia Tazania: Mpanju

Informações:

Sinopsis

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 18 COSP18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki kwenye Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa ulijadili ajenda mbalimbali za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuisha, kushirikishwa na kutoachwa nyumba. Amon Anastaz Mpanju Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo na aliketi chini na kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye alitaka kufahamu  ni nini kikubwa anachoondoka nacho kwenye mkutano huo kitakachofanyiwa kazi Tanzania na kuleta tija kwa watu wenye ulemavu.