Habari Za Un

26 JUNI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako mshikamano na wakimbizi unatekelezwa kwa vitendo na mashirika ya Umoja Mataifa likiwemo lile la Chakula na Kilimo (FAO) na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia Programu wa Pamoja ya Kigoma (KJP).Katika siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na usafirishaji haramu, ripoti mpya ya dunia ya Dawa za Kulevya mwaka 2025 iliyotolewa leo imeonya kuwa kutokuwepo kwa utulivu duniani kunachochea ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC, watu milioni 316 walitumia mihadarati mwaka 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly, amesema "Makundi haramu yanatumia migogoro kama fursa tunahitaji ushirikiano na uwekezaji kulinda jamii zetu.”Leo ni kumbukizi ya uzinduzi wa Chata ya Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita mjini San Francisco, hatua iliyoweka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 24, 1945. Katibu Mkuu António Guterres anasem