Habari Za Un
23 JUNI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:27
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu.Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambal