Habari Za Un
01 JULAI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:59
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika ukame na uhakika wa upatikanaji wa maji na kusikia jinsi taifa la Chile, linatumia sera kushawishi mabadiliko yanayoweza kukabiliana na tatizo hilo. Pia tunakuletea muhtasari na mashinani.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iran, Stefan Priesner amesema wanachofanya hivi sasa ni kupanga upya programu za Umoja wa Mataifa nchini humo wakimulika vipaumbele vipya kufuatia mashambulizi yaliyoanza tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu na kubadili mwelekeo wa kazi zao. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea Tehran mji mkuu wa Iran, Bwana Priesner amesema sasa tuko kwenye mazugumzo ya serikali kuona ni vipi tutapanga upya programu zetu kukidhi mahitaji mapya yanayoanza kuwa dhahiri, ikiwa ni siku chache tu tangu mashambulizi yakome baada ya sitisho la mapigano kuridhiwa.Huko huko Geneva, Uswisi lakini akizungumza kutoka Nairobi Kenya, Shaun Hughes, ambaye ni Mratibu wa Dharura kwa mzozo wa Sudan katika shirika la