Jua Haki Zako

Kenya : Vijana wazidi kuandamana

Informações:

Sinopsis

Kwa wiki za hivi karibuni zimekuwa za misukosuko nchini Kenya, mitaa ya jiji la Nairobi na miji mingine mikuu imekuwa ikifurika vijana… wakiwa na mabango mikononi, miili yao ikiwa tayari kwa chochote — hata kwa  gesi ya kutoa machozi  na risasi. Lakini maandamano haya yanamaanisha nini? Vijana hawa wanadai nini? Na wanaruhusiwa kisheria kufanya hivyo? Ndio maswali tutakayokuwa tunayajibu kwenye makala haya.   Karibu katika makala ya Jua Haki Zako – makala ambayo siku zote hukuelemisha kuhusu haki zako tena za msingi jina langu ni benson Wakoli