Siha Njema

Ukiwa utatembea hatua elfu saba kila siku unaweka magonjwa hatari mbali

Informações:

Sinopsis

Utafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na  kupoteza kumbu kumbu Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya. Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu. Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi  la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku. Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi. Wapo waliokuwa na wa