Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Sintofahamu yaendelea kuhusu kuanza kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na M23

Informações:

Sinopsis

Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; sintofahamu yaendelea kuhusu kuanza kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na Muungano wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Ukombozi wa Kongo AFC/M23, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na kujumuisha upinzani. Tutakueleza punde zaidi katika uchaguzi wa Tanzania. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi na eneo la Sahel, yasema hali ya usalama katika eneo hilo inasalia kuwa ya wasiwasi mkubwa na kimataifa Rais wa Marekani, Donald Trump, asema huenda hivi karibuni akakutana ana kwa ana na rais wa Urusi, Vladmir Putin, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.