Siha Njema

Kwa nini ni muhimu kuongeza uwekezaji bunifu katika afya ya watoto

Informações:

Sinopsis

Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika  imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla. Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu. Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu  wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu. Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo