Habari Za Un

Kutoka kufanya kazi za ndani hadi kumiliki kampuni ya usafi wa mazingira

Informações:

Sinopsis

Kutana na Godlove Makunge, kijana huyu wa kitanzania ambaye safari ya maisha  yake imedhihirisha kuwa chochote unachoweka nia na utashi kitafanikiwa. Godlove ambaye elimu yake ni ya kidato cha nne, hakuweza kuendelea na masomo zaidi. Alichukuliwa na mtu mmoja afanye kazi za ndani kutoka Morogoro hadi Lindi na kisha akaishia Mtwara, kusini-mashariki mwa Tanzania ambako huko aliona fursa ya kujipatia kipato kutokana na taka zilizokuwa zinasambaa mitaani. Aliasisi kampuni ya usafi na mazingira iitwayo Shikamana Investment. Sasa kampuni yao ya ubia imeajiri vijana 6. Alishiriki mafunzo ya uchumi rejeleshi yaliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP mkoani Mtwara. Sawiche Wamunza, Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati UNDP alizungumza na Bwana Makunge baada ya mafunzo hayo ili afahamu amejifunza nini.