Habari Za Un

13 AGOSTI 2025

Informações:

Sinopsis

Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nch