Habari Za Un

11 AGOSTI 2025

Informações:

Sinopsis

Jaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughu