Habari Za Un
07 AGOSTI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:51
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Jaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpang