Habari Za Un

06 AGOSTI 2025

Informações:

Sinopsis

Jaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, K