Habari Za Un

05 AGOSTI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi  kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva