Habari Za Un

01 AGOSTI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushi