Habari Za Un

31 JULAI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mik