Habari Za Un

IFAD: Kilimo chazaa matunda Rwanda: wakulima wadogo wajikwamua

Informações:

Sinopsis

Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Sharon Jebichii na  taarifa zaidi.