Habari Za Un
30 JULAI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:58
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiy