Habari Za Un
Türk ataka Israeli ishinikizwe iondoke maeneo inayokalia ya wapalestina
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:01:54
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKamishna Turk ameyasema hayo katika tarifa yake aliyoitoa kwa njia ya video kabla ya kuanza kwa mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani unaolenga kujadili Suluhu ya kudumu kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina ambao umedumu kwa miongo kadhaa sasa.Turk amesema: “Ninahimiza hatua za haraka za Israel kukomesha uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kwa pande zote kufanyia kazi maendeleo yanayoonekana kuelekea suluhu ya Serikali mbili.”Akatoa angalizo kwa zile nchi zitakazo shindwa kuweka shinikizo kwa Israel kukomesha mauaji huko katika Ukanda wa Gaza.“Nchi ambazo zinashindwa kutumia n