Habari Za Un

24 JULAI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika utapiamlo kwa watoto na madhila yasiyo fikirika  kwa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Kati, Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli. Pata pia muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana jinsi mitandao ya kihalifu duniani inavyoingiza kwenye masoko dawa za binadamu zenye viwango vya juu vya kemikali za sumu ambazo zimesababisha vifo na kuathiri afya ya wagonjwa wengi hasa watoto kwenye nchi za kipato cha chini.Tunasalia na afya ambapo hii leo WHO imethibitisha kwamba Timor-Leste imetokomeza ugonjwa wa malaria, hatua ya kipekee kwa nchi ambayo ilipatia kipaumbele malaria na kuanzisha juhudi za kitaifa na zilizoratibiwa mara tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 2002. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Volker Türk, amesema maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi ni ushindi