Habari Za Un

23 JULAI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Nigeria, na mradi wa nishati ya sola ya kusaidia wakulima nchini Ethiopia. Makala inakupeleka nchini Afrika Kusini na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata.Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia. Katika makalaShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama