Habari Za Un
16 JULAI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:59
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli; na ujumbe wa Uganda wa hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda Tanzania, kulinkoni?Amri mpya za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli kwa wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli zinazidi kuhatarisha maisha ya makumi ya maelfu ya watu ambao wameshahama mara kadhaa, wakiwemo wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma za kusafisha damu mwilini kila wiki.Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu, HLPF, la mwaka huu wa 2025 linaendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Wadau mbalimbali zikiwemo nchi zinazohudhuria zinabadilishana uzoefu, changamoto na mafaniko katika kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Mendeleo Endelevu, SDGs. Uganda imeeleza hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Makala tunasalia hapa