Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Mkutano wa pamoja kati ya SADC na EAC kuhusu DRC
08/02/2025 Duración: 20minKwa sehemu kubwa makala ya mtazamo wako imeangazia kuhusu hali ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mkutano wa pamoja kati ya jumuia ya Afrika mashariki EAC na jumuia ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo wa mashariki mwa DRC, huko Gabon upinzani umemtaka kiongozi wa mpito kuweka wazi msimamo wake kuhusu ushiriki wake katika uchaguzi mkuu, na hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kukata ufadhili kwa shirika la misaada USAID pia Marekani kudhibiti eneo la Gaza
-
Juhudi za kimataifa katika kusaka amani ya mashariki mwa DRC
01/02/2025 Duración: 20minMakala ya yaliyojiri wiki hii kwa sehemu kubwa imejikita katika kudadavua hali yausalama wa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako tangu mwanzo wa juma hili kulishuhudiwa mapigano makali kati ya jeshi la Nchi hiyo na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kwenye mji wa Goma, lakini pia siasa za mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania na maeneo mengine duniani
-
Kuapishwa kwa Rais wa Marekani Donald Trump kwa muhula wa pili
25/01/2025 Duración: 20minKuapishwa kwa Donald Trump kama rais wa 47 wa Marekani, Mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC, Tundu Lissu ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama cha Upinzani cha Chadema kule Tanzania, tutaangazia Sisa za Kenya, Sudan na maeneo Ya Afrika magharibi pia kwengineko duniani.
-
Israeli na wapiganaji wa Hamas wakubaliana kusitisha vita huko Gaza
18/01/2025 Duración: 20minMiongoni mwa yale tumekuandalia wiki hii ni pamoja na kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, mapigano yanyoendelea kuripotiwa mashariki ya DRC, makubaliano ya kusitishwa kwa vita kati ya Hamas na Israeli.