Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Afya ya kujifungua na uzazi: Changamoto zinazotokea wakati wa kujifungua mtoto
12/11/2024 Duración: 10minIdadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.
-
Afya ya uzazi na kujifungua
08/11/2024 Duración: 10minMakala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari nyepesi.Ni safari yenye changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.
-
Juhudi za kikanda kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka
29/10/2024 Duración: 08minKumekuwa na mikakati maksudi katika nchi za Afrika kuwekeza katika utafiti kuhusu nyoka na matibabu ya simu yake Baadhi ya mikakati hiyo ni utafiti wa kuwa na aina moja ya dawa ambayo inaweza kutumika katika nchi za Afrika Mashariki vile vile kuelimisha jamii kuhusu huduma za kwanza sahihi kuwasaidia wagonjwa na namna ya kuzuia madhara zaidi kutokana na sumu ya nyoka.
-
Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika
22/10/2024 Duración: 10minKungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.