Wimbi La Siasa

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 4:03:40
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episodios

  • Jaribio la mapinduzi nchini DRC lazua maswali mengi

    22/05/2024 Duración: 10min

    Wimbi la siasa inaangazia kilichotokea Mei 19 jijini Kinshasa ambako vikosi vya jeshi la serikali (FARDC) viilidai kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo.Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jumapili ya Mei 19, lakini sasa tukio hilo limeibua maswali mengi bila majibu. Kudadavua hili, utawasikia Georges Msamali, mtaalamu wa masuala ya kiusalama akiwa Nairobi nchini Kenya, Francois Alwende ni raia wa DRC na mtaalamu wa siasa za DRC.

  • Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi

    17/05/2024 Duración: 10min

    Kwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.

  • Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi

    10/05/2024 Duración: 10min

    Mazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba. Makundi haya ni yale yaliosusia mkataba wa amani wa mwaka 2018, wakati rais Salva Kiiri na hasimu wa wake wa kisiasa ambaye sasa ni makamo rais wa Kwanza Reik Machar walisaini mkataba wa amani.Soma piaKenya kuisaidia Sudan Kusini kupata suluhu ya utovu wa usalama wa miaka mingiKatika makala haya Benson Wakoli na wachambuzi wa kisiasa Fracis Wambete, ambaye na mhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, pamoja na Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka nchini Tanzania wanajaribu kuangazia kufaulu kwa mazungumzo haya, skiza.

  • Nini haki za wafanyakazi duniani ?

    01/05/2024 Duración: 10min

    Kila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutoka  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga

página 2 de 2