Sinopsis
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episodios
-
Hatua ya Marekani kujiondoa kwa mkataba wa Paris kuathiri nchi maskini
28/01/2025 Duración: 09minRais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa. Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa.Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.
-
Kenya: Jinsi nguo za mitumba zinachangia katika uharibifu wa mazingira
23/01/2025 Duración: 15minSekta ya mitumba inauwezo wa kuchangia mabilioni ya fedha katika mapato ya taifa, pamoja na kutoa maelfu ya ajira katika mataifa ya bara Afrika na ulaya. Kulinga na utafiti wa Oxford Econimics mwaka uliopita; 2024, sekta ya mitumba pekee ina dhamani ya dola bilioni 8 na imetoa ajiri ya idadi ya zaidi laki moja na elfu 60 kwa vijana nchini Msumbiji, Ghana na Kenya.Lakini hata hivyo wanaharakati wa mazingira wanasema baadhi ya nguo hizo za mitumba zinazoletwa Afrika zinachangia katika uchafuzi wa mazingira.Hili kufahamu Zaidi mwandishi wetu George Ajowi alizuru soko la Gikomba na kutuandalia makala yafuatayo .
-
Raia wakubali kuachana na matumizi ya kuni lakini nishati safi ni ghali kwao
15/01/2025 Duración: 09minMatumizi ya kuni yanaweza kuwa na athari chanya na hasi kwa mazingira, kulingana na jinsi zinavyovunwa, kutumiwa na kusimamiwa. Leo mwandishi Christopher Karenzi kutoka Kigali, Rwanda ameangazia hatua ya kuondokana na matumizi yake lakini changamoto pia raia wanazokumbana nazo.
-
Matumizi ya kilimo kinachokabili mabadiliko ya tabia nchi Afrika mashariki
07/01/2025 Duración: 10minMashirika kadhaa ya kilimo pamoja na serikali ya Kenya yaliwakutanisha wadau wa kilimo—wakulima, wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi, na watunga sera—jijini Nairobi mwezi Novemba mwaka uliopita. Mkutano huo ukilenga kuweka bayana mwelekeo wa kutumia kilimo kinachokabili mabadiliko ya tabianchi yaani climate smart agriculture ili kuongeza uzalishaji wa chakula.Hii leo katika makala mazingira leo dunia yako Kesho ,tunaangania kilimo hicho