Sinopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodios
-
Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka
25/10/2024 Duración: 09minNchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari. Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.
-
Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kike
24/10/2024 Duración: 10minKatika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani, tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.
-
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
18/10/2024 Duración: 09minSiku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia. Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.