Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:47:48
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • KENYA: Kuzaliwa, kufa na "kujaribu" kufufuka kwa mchezo wa masumbwi nchini Kenya.

    08/01/2025 Duración: 38min

    Popote pale ulipo nikukaribishe katika Makala ya jukwaa la michezo ndani ya FRI Kiswahili.Leo tumekuandalia Makala spesheli ambayo inaangazia kushuka pakubwa kwa viwango vya mchezo wa masumbwi nchini Kenya, Makala ambayo tunayapeperusha wiki kadhaa tu baada ya kukamilika kwa michezo ya Olimpiki Jijini Paris nchini Ufaransa. Kwa mara ya kwanza katika, historia ya kenya, hakuna bondia hata mmoja aliyewakilisha taifa katika michezo ya olimpiki jijini Paris. Hatua hii ilizua ngumzo kwa wadau wa mchezo huo.Lakini, Iweje mchezo uliokuwa ukisifika na kuiletea Kenya hadhi katika miaka ya nyuma imedidimia kiasi hiki? Je, ni usimamizi mbaya ama ni ukosefu wa ligi dhabiti au ni kukosa wadhamini wa kuwekeza katika mchezo hili kuiletea fahari inayostahili. Je, Kuna uhasama kati ya wadau ama wasimamizi wameingiwa na kiburi na kujisahau na kuwasahau mabondia?Mwenzangu George Ajowi amezungumza na Mabondia wa zamani, marefa, makocha, mapromota, wanahabari na vile vile wadau wengeni katika sekta hii na kuzungumza nao kuhusiana

  • Mashindano ya magari ya Dakar Rally 2025 yang'oa nanga huko Saudi Arabia

    04/01/2025 Duración: 23min

    Leo kwenye makala ya kwanza kabisa ya Jukwaa la Michezo mwaka 2025, tumeangazia raundi ya nne hatua ya makundi mechi za Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Mwanariadha mkenya Beatrice Chebet avunja rekodi yake ya dunia huku raia wa Eritrea mwendesha baiskeli Biniam Girmay akishinda tuzo la Afrika wakati uo huo mashindano ya magari ya Dakar Rally na Kombe la Mapinduzi yaking’oa nanga. Lakini pia tutatupia jicho tetesi za uhamisho ulaya na michuano ya tenisi ya Brisbane Open inayoendelea.

  • CAF: Niger, Sudan na Zambia zafuzu mashindano ya soka ya CHAN 2024

    28/12/2024 Duración: 23min

    Ikiwa Jumamosi ya mwisho ya mwaka 2024, tunakuuliza ni tukio gani au mashindano gani ya kispoti yalikufurahisha zaidi mwaka huu? Pamoja na hayo; tumeangazia kifo cha mchezaji nguli wa voliboli nchini Kenya Janet Wanja, Uganda yaibuka mabingwa wa CECAFA michuano ya kufuzu AFCON U17, raundi ya mwisho ya kufuzu michuano ya CHAN 2024, uchambuzi wa raundi ya 18 ya mechi za Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza. 

  • CHAN 2024: Rais Motsepe aridhishwa na maandalizi ya Kenya, Uganda na Tanzania

    21/12/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe Afrika Mashariki kuukagua maandalizi ya CHAN 2024, tuzo za wanasoka bora Afrika na FIFA mwaka huu, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury dhidi ya Oleksandr Usyk huku nduguye Paul Pogba, Mathias Pogba akipokea kifungo cha miaka mitatu jela kwa kujaribu kumlaghai Paul Pogba pesa.

página 2 de 2