Sinopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodios
-
Hofu kwa wafanyabiashara kuhusu muswada wa fedha 2024 nchini Kenya
29/05/2024 Duración: 10minMsikilizaji kwa wiki kadhaa sasa nchini Kenya, kumekuwa na mjadala mkali baada ya kutolewa kwa mapendekezo ya serikali kuhusu muswada wa fedha wa mwaka 2024 unaolenga kuongeza kodi katika baadhi ya sekta na bidhaa nchini humo.Wazalishaji na wawekezaji wakitarajiwa kuwa waathiriwa wakbwa ikiwa muswada huu utapitishwa kama ulivyo, ambapo baadhi ya vinavyolalamikiwa na wazalishaji ni nyongeza ya ushuru wa thamani katika malighafi kutoka nje pamoja na tozo za mazingira maarufu kama Eco Levy. Sekta ya uzalishaji wa viwanda inatarajiwa kuchangia asililia 20 katika pato ghafi la taifa hadi kufikia mwaka 2030. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, imezungumza na mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, Antony Mwangi, kuangazia changamoto na faida za muswada huu. Jina langu ni Emmanuel Makundi, karibu. Msikilizaji nilianza kwa kumuuliza Antony, wao wanautazamaje muswada huu? Insert /// Msikilizaji kama umeungana nasi Makala ni Gurudumu la uchumi na leo tunaujadili muswada wa fedha nchini Kenya unaoelnga
-
Afrika na jitihada za kutaka kuwa katika meza ya majadiliano ya kidunia na sio mualikwa
22/05/2024 Duración: 10minMsikilizaji wakati wa kongamano la kimataifa la wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali duniani waliokutana nchini Rwanda, maswali kadhaa yaliibuliwa, kubwa lilikuwa ni je bara la Afrika linapaswa kuwa katika meza ya maamuzi au kwenye orodha, na ikiwa huu ni muda muafaka wa kutoa mustakabali wake. Ni maswali magumu ambayo hata hivyo viongozi wa Afrika walioshiriki, wanakubaliana kuwa bara hili lina rasilimali zakutosha kubadili uelekeo wake na maendeleo kwa raia, lakini pia halipaswi kuwa linaomba kwa viongozi wa magharibi kuwa katika meza ya majadiliano kuhusu mustakabali wa uchumi na maendeleo ya dunia. Suala la mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa mkataba wa biashara huria wa bara hili, maarufu kama AfCFTA, liliibuka, ambapo licha ya utiwaji saini itifaki yake, bado kuna vikwazo vya kufanya biashara baina ya nchi za Afrika.
-
Changamoto na fursa kwa vijana wajasiriamali na ajira kwenye nchi za Afrika Mashariki
15/05/2024 Duración: 09minHujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Takwimu za hivi karibuni za benki ya dunia zinaonesha uhalisia wa tatizo, takwimu zikitofautiana baina ya nchi na nchi, lakini kiujumla ni kuanzia kati ya asilimia 4 hadi 19 ya vijana hawana ajira, huku wanawake walioko vijijini wakiwa waathirika wakubwa. Katika makala haya hivi leo, tutaangazia kwa kina namna gani bora ya kukabiliana na tatizo la ajira na kuongeza wajasiriamali wengi zaidi kwenye ukanda. Kwenye line ya simu nimewaalika, Ali Mkimo, yeye ni mchambuzi wa masuala ya Uchumi pamoja na Emmanuel Cosmas, kijana mbunifu wa masuala teknolojia na nibalozi wa UNICEF, wote hawa wakiwa nchini Tanzania.
-
Mchango wa biashara ndogondogo na kati kwa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki
10/05/2024 Duración: 08minMakala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia mchango na changamoto ya biashara ndogondogo na zile za kati kwenye nchi za Afrika Mashariki.Matayarishaji amezungumza na wafanyabiashara wadogowadogo na kati nchini Kenya, lakini mchambuzi wa masuala ya uchumi Ally Mkimo.