Sinopsis
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episodios
-
Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024
13/10/2024 Duración: 20minAli Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.
-
Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini Kenya
06/10/2024 Duración: 19minMakala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wameru kutoka nchini Kenya, wapo pia nchini Tanzania.
-
Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2
29/09/2024 Duración: 20minkaribu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania