Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno KUTOHOA
03/07/2025 Duración: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.
-
03 JULAI 2025
03/07/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini Uganda katika Mbuga ya Wanyama inayofahamika kwa jina Murchison Falls National Park kuangazia namna washiriki wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika mapema mwaka huu jijini Kampala walivyofurahia mazigira asili nchini Uganda na namna yanavyounufaisha ulimwengu.Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa maendeleo umemalizika leo huko Sevilla, Hispania ambapo mashirika ya kiraia yametaka utekelezaji kwa vitendo kwa yale yaliyomo katika nyaraka iliyopitishwa iliyopatiwa jina Makubaliano ya Sevilla.Mmoja wa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, Paula Sevilla amesema kinachohitajika ni uongozi kutoka nchi tajiri ambako ndiko zilizko kampuni kubwa zinazokwepa kodi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kuhusu vijana na mifumo ya uzalishaij chakula na kilimo inaonesha kuwa karibu asilimia 85 ya vijana duniani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati, ambako mifumo hiyo ni muhimu kwa ajira
-
UNDP Tanzania yahimiza ubunifu wa vyanzo vya mapato ili kuvutia wawekezaji
02/07/2025 Duración: 03minMkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii. Lengo ni kuendelea kuunga mkono serikali na wadau mbalimbali barani Afrika katika kutafuta mbinu mbadala za kufadhili maendeleo.Sharon Jebichii na maelezon zaidi.
-
IOM yasema uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji ni muhimu
02/07/2025 Duración: 01minKatika Mkutano wa nne wa kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
-
02 JULAI 2025
02/07/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia wahamiaji na njia bunifu ya kuwawezesha kujikimu kimaisha, na malezi bora ya watoto nchini Tanzania. Makala tunasalia huko huko Tanzania kumulika uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya.Katika Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa..Katika makala mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukikunja jamvi leo huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu
-
UNICEF Tanzania: Nidhamu chanya huchagiza makuzi bora kwa mtoto
02/07/2025 Duración: 01minShirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa.
-
01 JULAI 2025
01/07/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika ukame na uhakika wa upatikanaji wa maji na kusikia jinsi taifa la Chile, linatumia sera kushawishi mabadiliko yanayoweza kukabiliana na tatizo hilo. Pia tunakuletea muhtasari na mashinani.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iran, Stefan Priesner amesema wanachofanya hivi sasa ni kupanga upya programu za Umoja wa Mataifa nchini humo wakimulika vipaumbele vipya kufuatia mashambulizi yaliyoanza tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu na kubadili mwelekeo wa kazi zao. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea Tehran mji mkuu wa Iran, Bwana Priesner amesema sasa tuko kwenye mazugumzo ya serikali kuona ni vipi tutapanga upya programu zetu kukidhi mahitaji mapya yanayoanza kuwa dhahiri, ikiwa ni siku chache tu tangu mashambulizi yakome baada ya sitisho la mapigano kuridhiwa.Huko huko Geneva, Uswisi lakini akizungumza kutoka Nairobi Kenya, Shaun Hughes, ambaye ni Mratibu wa Dharura kwa mzozo wa Sudan katika shirika la
-
Vijana wakumbatia kilimo bunifu kupambana na mabadiliko ya tabianchi Kajiado nchini Kenya
30/06/2025 Duración: 03minKwa mujibu wa wataalamu wa kilimo, teknolojia imefungua njia mpya ya kuinua maisha ya wakulima wadogo, hasa kwa kutumia ukulima wa kisasa unaotumia maarifa na Teknolojia. Sharon Jebichii anatupeleka kaunti ya Kajiado, Kenya, katika eneo la EMbulbul, kukutana na vijana wanaotumia maarifa ya kilimo cha kisasa kubadilisha maisha yao na ya jamii.
-
Guterres awaambia viongozi wa dunia huko Sevilla Ni wakati wa kufadhili mustakabali wetu na kubadilisha mwelekeo
30/06/2025 Duración: 02minMkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa. Anold Kayanda amefuatilia na anatupasha zaidi
-
30 JUNI 2025
30/06/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 huko Sevilla Hispania, na siku ya Mabunge tukizungumza na mmoja wao kutoka Tanzania. Makala inatupeleka nchi Kenya na mashinani tunarejea huko huko Tanzania, kulikoni?Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti..Katik
-
Siku ya mabunge duniani - Harakati za Usawa wa kijinsia Tanzania
30/06/2025 Duración: 02minLeo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti.
-
UNICEF Kenya - Elimu Jumuishi kupitia michezo: Watoto wenye ulemavu wa kuona wapate nafasi sawa
27/06/2025 Duración: 03minKatika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya ulemavu wa uziwi na kutoona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya. Sharon Jebichii na makala zaidi.
-
Kilichotokea nchini Burundi 1972-1973 ni mauaji ya kimbari jumuiya ya kimataifa itambue hilo: Ndayicariye
27/06/2025 Duración: 02minSerikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa? Flora Nducha anatujuza zaidi
-
27 JUNI 2025
27/06/2025 Duración: 09minHii leo jaridanitunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na mauaji yaliyofanyika nchini Rwanda kati ya mwaka 1972 hadi 1973. Makala tunamulika inayochukuliwa nchini Kenya za kutekeleza haki za watu wenye ulemavu wa kutoona, na mashinani tunakwenda DRC, kulikoni?Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya viziwi wasioona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea
-
WHO yasema vifaa vya matibabu vimeingia Gaza lakini bado havitoshi
27/06/2025 Duración: 02minHatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno AFRITI KIJITI
26/06/2025 Duración: 36sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI.”
-
26 JUNI 2025
26/06/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako mshikamano na wakimbizi unatekelezwa kwa vitendo na mashirika ya Umoja Mataifa likiwemo lile la Chakula na Kilimo (FAO) na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia Programu wa Pamoja ya Kigoma (KJP).Katika siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na usafirishaji haramu, ripoti mpya ya dunia ya Dawa za Kulevya mwaka 2025 iliyotolewa leo imeonya kuwa kutokuwepo kwa utulivu duniani kunachochea ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC, watu milioni 316 walitumia mihadarati mwaka 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly, amesema "Makundi haramu yanatumia migogoro kama fursa tunahitaji ushirikiano na uwekezaji kulinda jamii zetu.”Leo ni kumbukizi ya uzinduzi wa Chata ya Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita mjini San Francisco, hatua iliyoweka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 24, 1945. Katibu Mkuu António Guterres anasem
-
UN80: Umoja wa Mataifa wajitathmini kwa ajili ya karne mpya
25/06/2025 Duración: 03minKatika dunia inayokumbwa na migogoro inayoendelea kuongezeka, kupanuka kwa pengo la usawa, na kupungua kwa imani katika taasisi za kimataifa, Umoja wa Mataifa umeanzisha juhudi kabambe za kuboresha namna unavyowahudumia watu kote ulimwenguni. Mpango wa UN80, uliotangazwa mwezi Machi na Katibu Mkuu António Guterres, ni juhudi ya mfumo mzima inayolenga kurahisisha utendaji kazi, kuongeza ufanisi, na kuthibitisha tena umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika kwa kasi. Je nini nini kinatarajiwa katika mpango huo wa UN80? Ungana na Flora Nducha katika Makala hii
-
Wanawake wa Somalia: Uongozi wenu, dira na ujasiri ni msingi wa mustakabali wa Somalia
25/06/2025 Duración: 02minNchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.
-
Upatikanaji wa nishati duniani umeboreka lakini uwezeshaji kifedha bado unahitajika kupunguza tofauti – Ripoti ya UN
25/06/2025 Duración: 02minRipoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.