Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:54:46
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali vitaikomboa Afrika kimaendeleo: Vijana Kenya

    04/04/2025 Duración: 03min

    Majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu w anchi na serikali, wadau wa maendeleo na vijana. Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid je wanasemaje? Ungana nao katika makala hii

  • Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini

    04/04/2025 Duración: 01min

    Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

  • 04 APRILI 2025

    04/04/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha u

  • Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS

    04/04/2025 Duración: 02min

    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MHARUMA.”

    03/04/2025 Duración: 31s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MHARUMA.”

  • 03 APRILI 2025

    03/04/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha kwenye mkutano wa hivi majuzi wa CSW69 kufuatilia harakati za Mfuko wa CRDB za kujengea uwezo na kuinua wanawake nchini Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno “MHARUMA.”Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu leo wamesema wanaendelea kuwasaidia watu wa Muyanmar na mahitaji ya msingi baada ya tetemeko kubwa la ardhi la Ijuma iliyopita ambapo idadi ya waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 2,800, maelfu wamejerihiwa na mamia bado hawajulikani wako.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema leo kwamba ameshtushwa na ripoti za mauaji ya raia bila kufuata utaratibu wa kisheria yaliyoenea mjini Khartoum baada ya kurejeshwa kwa mji huo chini ya udhibiti wa Jeshi la Sudan (SAF) tarehe 26 Machi.Na majadiliano ya siku mbili ya kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madrid yameanza leo Nairobi Kenya mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo. shudu

  • UN na wadau wasadie chanzo cha usonji kifahamike - Lukiza Foundation

    02/04/2025 Duración: 04min

    Hii leo dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usonji, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Foundation nchini Tanzania inayoelimisha umma kuhusu usonji.  Usonji ni hali inayompata mtoto au utofauti au changamoto katika mfumo wake wa ufahamu na ubongo na kusababisha changamoto za kimawasiliano, tabia na kudhibiti hisia mwili. Hoja kubwa ni kwamba hadi sasa sababu ya hali hiyo kumpata mtoto  haijajulikana na ndipo taasisi hiyo inachagiza  Umoja wa Mataifa na wadau washikamane katika tafiti kujua chanjo kama njia mojawapo ya kudhibiti au kutibu ugonjwa huo. Basi kwa kina kufahamu harakati za taasisi hiyo nchini Tanzania, nampisha Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

  • Ujumbe wa Katibu Mkuu UN Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma Kuhusu Usonji

    02/04/2025 Duración: 01min

    Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote. Anold Kayanda anaeleza zaidi.

  • 02 APRILI 2025

    02/04/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji, na wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Tanzania kwa mada hiyo hiyo ya elimu kuhusu usonji, na mashinani tunakwenda Gaza.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote.Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha.Makala leo kama tulivyokujulisha ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umm

  • Stadi za kuoka mikate zaleta furaha kwa mkimbizi Thérèse huko Beni nchini DRC

    02/04/2025 Duración: 01min

    Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha. Sharon jebichii na taarifa zaidi.

  • Tanzania: UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo

    28/03/2025 Duración: 01min
  • Tetemeko la ardhi barani Asia, UN yatuma salamu za rambirambi

    28/03/2025 Duración: 01min
  • 28 MACHI 2025

    28/03/2025 Duración: 09min

    Umoja wa Mataifa watuma salamu za rambirambi kufuatia tetemeko barani Asia.UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo, Tanzania.Makala ni kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kutozalisha Taka.Mashinani tunamulika ubunifu wa Janet Chemitei  wa Tengeneza Cafe katika urejelezaji nguo nchini Kenya.

  • METHALI: NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI

    27/03/2025 Duración: 01min

    Karibu kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani na anafafanua methali Ndoto njema haihadithiwi.

  • 27 MACHI 2025

    27/03/2025 Duración: 11min

    Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunaendelea na kuwasikia wadau waliohudhuria mkutano uliomalizika wiki iliyopita wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW69 unaotathmini Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji vilivyopitishwa mwaka 1995 katika mkutano wa 4 wa kimataifa wa wanawake huko Beijing China. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili ambapo leo utapata ufafanuzi wa methali "NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI"

  • Chad: Wanakikundi watumia faida ya biashara yao kuanzisha shule

    26/03/2025 Duración: 03min

    Nchini Chad, wanawake wanakikundi cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupata mwilini wameamua kuchukua hatua ili umamuma wa kutokujua kusoma na kuandika ambao umewakumba wao, usiwakumbe pia watoto wao wa kike. Wanakikundi hao wa APROFiCA wanaopata ufadhili kutoka Benki ya Dunia wameona ni vema kuchukua hatua hiyo ili kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, kwani elimu ni mkombozi kwa binadamu. Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua kupitia video ya Benki ya Dunia.

  • UN: Hali inazidi kuwa tete Gaza huku watu zaidi ya milioni wakiwa hatarini kukosa mlo

    26/03/2025 Duración: 02min

    Watu zaidi ya milioni 1 wako katika hatari ya kukosa chakula endapo misaada haitoruhusiwa kuingia Gaza wakati huu mashambulizi makali ya Israel yakizidisha janga la kibinadamu yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • 26 MACHI 2025

    26/03/2025 Duración: 11min
  • Baada ya kukimbilia Burundi, wakimbizi wa DRC wakubwa na uhaba wa mahitaji muhimu

    26/03/2025 Duración: 02min

    Hali ya kibinadamu ya wakimbizi zaidi ya 100,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokimbilia nchini Burundi kusaka usalama kutokana na mapigano mashariki mwa nchi yao katika katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, iliyopita ni ya mashaka, wakati huu ambapo ufadhili unazidi kukumbwa na mkwamo, wakikabiliwa na uhaba wa huduma kama chakula, huku kukiwa na pengo la ufadhili. Je ni madhila yapi?  Sharon Jebichii anafafanua zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

  • 25 MACHI 2025

    25/03/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki

página 1 de 5