Sinopsis
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episodios
-
Matumizi ya viuatilifu au viuadudu na madhara kwa mazingira
01/07/2025 Duración: 10minHatua ya serikali ya Kenya kuoiga marufuku matumizi ya takriban viuatilifu au dawa za kuua wadudu takriban 77 kutokana na hofu ya usalama wa dawa hizo kwa mazingira na afya ya binadamu. Baadhi ya viuatilifu vimepigwa marufuku katika soko la kimataifa, kuanzia baranai ulaya, Australia, marekani na Canada, laini viipo kwenye masoko ya nchi za ukanda.
-
Vitabu: Kampeni ya kuwafikia watoto milioni moja kuhusu uhifadhi
23/06/2025 Duración: 10minWatoto wana jukumu muhimu katika uhifadhi wa mazingira na wanyamapori kwa kushiriki kikamilifu katika mipango kama vile kupanda miti, udhibiti wa taka, na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mazingira na wanyamapori. Kuwashirikisha watoto katika shughuli hizi kunakuza hisia ya uwakili, kuwaunganisha na mazingira wanayoishi, na kukuza mazoea endelevu kwa siku zijazo.
-
Mgogoro wa Bahari: Afrika yataka kushirikishwa kikamilifu katika ulinzi wa bahari
19/06/2025 Duración: 10minMkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kutekeleza lengo nambari 14 la Maendeleo Endelevu, ulifanyika kule Nice, Ufaransa, kujadili mbinu mwafaka za kuhifadhi na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake, washikadau wakiunda uhusiano mpya kati ya wanadamu na mazingira ya baharini. Mkutano wa kilele ulikamilika Ijumaa tarehe 13 Juni, 2025 wakati huu mataifa yakitarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili sheria za uchimbaji madini kwenye kina kirefu cha maji baharini.
-
Mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa bahari wang’oananga jijini Nice, Ufaransa
09/06/2025 Duración: 10minMataifa yametakiwa kuchukua misimamo mikali kuhusu uvuvi wa kupindukia, uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini.
-
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Mazingira, taka za plastiki suala kuu
02/06/2025 Duración: 10minUchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.
-
Je dunia iko katika njia sahihi kutimiza lengo la kumaliza njaa kufikia 2030?
26/05/2025 Duración: 09minJumatano ya Mei 28 2025, dunia itaadhimisha siku ya njaa ulimwenguni, siku hii ikilenga kutoa hamasa na kuchochea hatua kuchukuliwa ili kumaliza njaa duniani. Kulingana na ripoti ya kimtaifa ya 2025 kuhusu migogoro ya Chakula, zaidi ya watu milioni 295.3 katika nchi 53 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.
-
Uchakataji wa plastiki katika kuhifadhi mazingira ya bahari na kupata mapato
15/05/2025 Duración: 09minJamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.
-
Mabadiliko ya tabianchi: Hali ya mifumo ya sheria katika suhughulikia ukatili wa kijinsia.
05/05/2025 Duración: 10min -
Mabadiliko ya tabianchi yachochea ongezeko la ukatili wa kijinsia
28/04/2025 Duración: 10minRipoti hiyo mpya ya UN Spotlight initiative, imebaini kuwa mabadiliko yatabianchi yameendelea kuzidisha mogogoro ya kijamii na kiuchumi ambayo inachochea kuongezeka kwa viwango vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.
-
Cha kutarajiwa katika ahadi mpya za nchi za kukabili mabadiliko ya tabianchi
23/04/2025 Duración: 10minRipoti ya umoja wa mataifa inaonesha dunia ipo nyuma sana katika kudhibiti ongezeko la joto chini ya nyuzi joto 1.5.
-
Mbolea asilia: Suluhisho kwa uharibifu wa udongo na changamoto za kilimo Kenya
14/04/2025 Duración: 10minBaadhi ya wakulima nchini Kenya wameanza kugeukia matumizi ya mbolea asilia inayonyunyiziwa ardhini ili kunusuru mashamba yao.
-
Mabadiliko ya tabianchi yahatarisha barafu ya milimani, barafu hii ikiyeyuka kwa kasi
31/03/2025 Duración: 10minKutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa duniani WMO, barafu inayopatikana kwenye milima inayeyuka kwa kasi zaidi na ndio sababu ya umoja wamataifa kutenga Machi 21 kama siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu kuyeyuka kwa barafu hii.
-
Juhudi zinazofanywa na wadau kufadhili wakulima wadogo barani Afrika
28/03/2025 Duración: 10minWakulima wadogo wanachangia kwa zaidi ya asilimia 70 uzalishaji wa chakula barani Afrika, hii ni kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo barani, Afdb, wakati uo huo, lengo nambari mbili ya maendeleo endelevu ikinuia kumaliza njaa na kuihakikishia dunia usalama wa chakula kufikia mwaka wa 2030
-
Raundi ya tatu ya mataifa kuwasilisha ahadi zao za kitaifa, NDCs za kukabili mabadiliko ya tabianchi
17/03/2025 Duración: 10min -
Siku ya wanayampori: Jinsi binadamu hutegemea rasilimali za wanyamapori na bayoanuwai.
11/03/2025 Duración: 10minBinadamu hutegemea rasilimali za wanyamapori na bayoanuwai ili kukidhi mahitaji yao. Tunahitaji chakula, mafuta, makazi, na hata mavazi. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kwamba mifumo ikolojia inaweza kustawi na mimea na wanyama wanaweza kuwepo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Machi 3 mwaka huu, ilikuwa ni fursa ya kutoa uhamasisho wa umuhimu wa wanyama na mimea pori, ili kuongeza ufahamu wa faida zao, na haja ya kuongeza mapambano ya uhalifu dhidi ya wanyamapori na kusababisha athari kubwa za kiuchumi, mazingira na kijamii.Skiliza ufahamu mengi zaidi.
-
Utupaji salama wa taka za kieletroniki, mashirika yachangamkia fursa kuokoa mazingira
04/03/2025 Duración: 09minTaka za kieletroniki zinajumuisha vitu vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira na utupaji ovyo ni chanzo kikuu cha madhara, dutu hizi hatari zikiwa na uwezo wa kuchafua udongo, maji, hewa na vyanzo vya chakula. Shirika la E-Waste Initiative Kenya linatoa suluhu ya taka za kieletroniki. Bonyeza hapa kufahamu zaidi.
-
Mwali wa mwisho: Mkaa wa Briketi kama suluhu ya nishati jadidifu
20/02/2025 Duración: 09minMkaa wa Briketi hutengenezwa kutoka kwa vumbi la mkaa wa kawaida, taka za kilimo au mabaki ya mbao, na hutumiwa kimsingi kwa mapishi nyumbani, shuleni na hata katika makampuni. Mkaa huu una faida kwa kuwa unapunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza ukataji wa miti lakini pia huwaka kwa muda mrefu na kwa usawa zaidi kuliko mkaa wa kawaida, na kuufanya kuwa chaguo maarufu kwa kupikia.
-
Umuhimu wa matumizi ya madawa ya kiasili kunyunyuzia mimea shambani
10/02/2025 Duración: 10minMakala haya yanazungumzia jinsi Wakulima wengi nchini Kenya wanakumbatia mbinu mpya za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea kwa kutumia madawa ya kiasili badala ya kemikali za viwandani. Kutokana na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kemikali,wakulima hawa sasa wanageukia madawa hayo asilia kuimarisha mazao na mazingira , Mimea kama vile ,pareto,kitunguu saumu,pilipili na hata mtunguja pori yaani sodom apple sasa inatumika kutengeneza madawa hayo.
-
Wakaaji wa mijini wanavyotumia Bustani ya Nyumbani kukabili mabadiliko ya tabia nchi
03/02/2025 Duración: 09minUtunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo.Bustani hii hutumika kwa kilimo cha mboga, viungo vya upishi kama vitunguu, matunda, au mimea ya kitiba kwa matumizi.
-
Hatua ya Marekani kujiondoa kwa mkataba wa Paris kuathiri nchi maskini
28/01/2025 Duración: 09minRais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa. Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa.Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.