Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Nchini Kenya CAF yadhibiti idadi ya mashabiki viwanjani kwenye michezo ya chan
12/08/2025 Duración: 10minMada ya leo ni kuhuus michuano ya CHAN inapoendelea kushika kasi kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, nchini Kenya baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani bila ya tiketi, hatua ambayo shirikisho la soka la Afrika CAF, limelazimika kupunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani kwa sababu za kiusalama.,,tumemuuliza nini kifanyike kudhibiti usalama wa mashabiki na viwanja? na Kwenye nchi yako wakati wa mechi kubwa hali huwaje?
-
Leo ikiwa ni siku ya ijumaa tarehe 08 08 2025 huwa ni mada huru .
08/08/2025 Duración: 10minLeo ni siku ya mada huru. Tunampa nafasi mskilizaji kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwake wiki hii,na pia anaweza kuzungumzia kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya juma hili.
-
Hatua ya wanasiasa kuhama hama vyama baada ya kukosa kufaulu kwenye uteuzi
07/08/2025 Duración: 10minmada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
-
Majadiliano ya Geneva kuhusu hatua za kukabiliana na matumizi ya plastiki
06/08/2025 Duración: 10minWawakilishi kutoka kote duniani wanakutana, wako Geneva, kujadili hatua za mwisho za kukabiliana na matumizi ya bidhaa za plastiki ambazo zimeendelea kuharibu mazingira.Tumemuuliza msikilizani ni njia zipi mbadala zitumike badala ya bidhaa za plastiki na anafikiri ni kwa nini nchi hazitaki kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.
-
-
Viongozi wakutana Ethiopia kujadili usalama wa njaa baa la njaa likishamiri
29/07/2025 Duración: 09min -
Msururu wa mashambulizi ya AL shabab nchini Somalia yanavyohujumu usalama
29/07/2025 Duración: 08minAl Shabab imezidisha mashambulizi yake na kuiteka miji zaidi wakati vikosi vya umoja wa Afrika vikitarajiwa kuondoka
-
-
Tishio la kuzuka mzozo mpya kati ya Eritrea na Ethiopia kuhusu eneo la bahari
22/07/2025 Duración: 09minRais wa Eritrea Isaias Afwerki ameionya Ethiopia dhidi ya kuzuka tena kwa mzozo kwa kulazimisha kutumia eneo lake ya Bahari.
-
Afrika yaendelea kuathirika kufuatia hatua ya Marekani kusitisha misaada
21/07/2025 Duración: 10minNchini Zimbabwe wataalam wanasema wagonjwa wa Malaria wanaongezeka kwa kasi tangu Marekani kupitia shirika lake la USAID kukatisha misaada yake kwa nchi hiyo na bara la Afrika
-
Kenya yaondoa ulazima wa viza kwa mataifa ya Afrika isipokuwa Somalia na Libya
18/07/2025 Duración: 10min -
-
Marais wa Afrika kusalia madarakani kwa muda mrefu hata umri ukiwa umeenda
15/07/2025 Duración: 09min -
-
Kila Ijuma unapata nafasi kuchangia chochote ndani ya rfi Kiswahili
15/07/2025 Duración: 09minKila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote ile kwenye makala haya. Skiza maoni ya waskilizaji.
-
Kenya : Maandamano yatumika kupora mali
15/07/2025 Duración: 09minMaandamano nchini Kenya na mataifa mengine ya Afrika yamekumbwa na mauaji na uporaji huku mali za watu zikiharibiwa. Je, unafikiri ni sahihi kwa waandamanaji kupora na kuharibu mali za watu? Nini vyombo vya usalama vinapaswa kufanya kuzuia uharibifu? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Viongozi wa Afrika wanatuhumiwa kuahidi mengi wakati wa kampeni na kutotimiza
14/07/2025 Duración: 09min -
Kenya: Mahakama ya juu yasema mwana haramu si haramu
09/07/2025 Duración: 09minKatika makala haya tujadili hatua ya mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, kuagiza kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kwenye dini ya kiislamu ana haki ya kumiliki mali ya babake kama watoto wengine waliozailiwa ndani ya ndoa, hatua inayoenda kinyume kabisa na tamaduni za dini hiyo. Unazungumziaje uamuzi huu wa mahakama nchini Kenya ? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Côte d'Ivoire : Kurejeshewa ngoma maalum kutoka Ufaransa
08/07/2025 Duración: 09minKaika makala haya tunajadili hatua ya bunge nchini Ufaransa kupiga kura na kupitisha mswada wa kurudishwa nchini Ivory Coast ngoma maalum inayozungumza iliyochukuliwa katika nchi hiyo ya Afrika kutoka kabila la Ebrie wakati wa ukoloni mwaka 1916. Je umefika wakati kwa koloni za zamani za Bara la Afrika kurejesha vyombo walivyopora ? Ndilo swali tumekuuliza . Haya hapa maoni yako.
-
Siku ya lugha ya kiswahili duniani makala maalum
07/07/2025 Duración: 10minSiku ya kiswahili duniani, ambayo imekuwa ikiadhimishwa tangu mwaka 2022. Maadhimisho ya mwaka huu imefanyika jijini Kigali nchini Rwanda, ambako mamia ya wataalam na wapenzi wa Kiswahili wamekutana kwa siku mbili kujadiliana kuhusu nafasi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa raia wa nchi zote za Jumuiya. Kauli mbiu ni kusherehekea lugha ya Umoja, utambulisho na mchango wake kwa dunia.RFI kiswahili imeshirikiana na taasisi ya mafunzo ya biashara na ufundi stadi, NIBS ya jijini Nairobi, kuandaa makala maalum ya Habari RAFIKI na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameongoza makala hii